Baada ya msanii wa muziki Roma Mkatoliki kupotea katika mazingira ya kutatanisha akiwa katika studio ya Tongwe Records
wasanii mbalimbali wameonesha kuguswa na kuamua kutumia mitandao yao ya
kijamii kuonesha masikitiko yao, Leo April 7 kupitia mtandao wa
Instagram Idriss Sultan alikua na haya ya kusema,
Hawa ni wasanii na ni maarufu,
sitamani kujua ni wangapi tusiowajua waliopotea katika mfumo kama huu.
Nina hofu sio kwa maisha yangu na uhuru wangu ila kwa kaka, dada,
watoto, baba, mama na ndugu , wake, waume, na wapenzi wa watanzania
wenzangu wasio na sauti niliyo nayo mimi –Idris Sultan
Mwenyezi Mungu hakunipa
nilichonacho ili niishie kupimisha misuli na wenzangu nani zaidi, watu
kama mimi ndio wa kwenda motoni haraka zaidi tukishaulizwa ulifanyia
nini ulichopewa. Raisi Magufuli, waziri Mwakyembe na Mkuu wa mkoa
Makonda nina imani hili lipo mezani kwenu naombeni mlitolee tamko zaidi
ya “Uchunguzi unafanyika” –Idris Sultan
pia mlivalie njuga kuwapata ndugu
zetu ili kutuliza amani ya hii nchi iliyopiganiwa iliyokuzwa kwa upendo
na amani ya juu kabisa. We can’t call it the land of peace wakati
ukilala hujui kama utaaamka sehemu unayoijua na ukiwa hata na hali yako
ya kiafya ile ile. –Idris Sultan
Leo ni Roma na Moni, kesho ni nani ?
Kamanda Sirro sijasahau kabisa usalama wa huu mji upo mikononi mwako.
Wake za hawa wawili wanaongea na watoto wao wanawaambia baba yupo ila
amesafiri anarudi kesho. Kesho isipofika basi inshaallah tutajua
Tanzania yetu ni nchi ya aina gani. Hata Mungu simuachii hili
hatujalishindwa bado –Idris Sultan
CHANZO CHA HABARI NA: millardayo.com
Endelea kuitembelea DJ WILLKAN BLOG
kwa kulike Page yetu ya Facebook,..DJWillkan.com, pia Instagram: @djwillkan_zekanvol
tufollow pia Twitter: @Djkanvol
No comments:
Post a Comment