Uzinduzi wa Albam ya Video ya 'Asante Yesu' utakaofanyika 29 Novemba katika Kanisa la A.I.C KAMBARAGE Mjini Shinyanga, Kuanzia saa 8:00 mchana. Asante Yesu ni Albam ya zamani sana ambayo imesheheni nyimbo nyingi, kama vile NG'WANA NJIMEJI, ELIAH, HELI YA MWAKA MPYA na zingine nyingi.
Kwanini wameamua kuzirudia nyimbo hizi?
Ni baada ya wapendwa wao kuzihitaji sana nyimbo hizi katika upande mwingine wa Video na pia ni kutunza kumbukumbu, maana nyimbo hizi au kwaya hii ya A.IC KAMBARAGE inahistoria ndefu tangu ilipo anzishwa mwaka 1989 Tar 12 Mwezi 07, ikiongozwa na Mwalimu wao wa kwaya ALEX BULUGU.
Kuanzishwa kwa kwaya ya A.I.C KAMBARAGE,
Tar 12/07/1989 kwaya hii ndio alianzishwa baada ya kutoka kwa Mungu hakuna Mzee, Hadi kufikia sasa imetimiza miaka 25. Wimbo wa 'ASANTE YESU' ulirekodiwa mwaka 1996, baada ya kupata Ajali mbaya sana katika Bonde la Ufa Tar 28/12/1995, Nchini KENYA, wakati wakitoka Kenya katika mwaliko maalum walioalikwa na Raisi Moi.
Alex Bulugu ambaye ndiye alikuwa mwalimu wa kikundi hicho cha kwaya, ambaye kwa sasa ni marehemu. Aliamua kukaa chini na kuandika shukurani kwa Mungu na ndipo akaona haina budi kumshukuru muumba wa mbingu na nchi, na ndipo ilipopatikana 'ASANTE YESU' Mwaka 1996 katika Studio za Babtist Nchini Kenya.
Wapendwa wao walituma maombi mengi sana kutokana ujumbe mzuri wa nyimbo hizo. A.I.C KAMBARAGE CHOIR walianza kurekodi Albam ya kwanza ya Video;
1. PIGA KELELE,
2. UTANDAWAZI,
3. SHETANI KAMA BUIBUI.
ALBAM ya 4 ambayo 29 Novemba ndio inakwenda kuzinduliwa inaitwa 'ASANTE YESU'.
Wote mnakaribishwa sana njoo ujipatie nakala yako,
usingoje kusimuliwa.
djwillkan.blogspot.com
No comments:
Post a Comment