Mshindi wa kwanza katika kinyang'anyiro hicho ni bi Nicole Franklyn Sarakikya kutoka wilaya ya Kishapu,mshindi wa pili ni Mary Emmanuel kutoka Ushetu,mshindi wa tatu ni Rachel Judica kutoka Shinyanga vijijini ,mshindi wa nne ni Nyangi Warioba kutoka Msalala, na mshindi wa 5 Neema Kakimpa kutoka wilaya ya Kahama |
Mshindi
wa taji la Redd's Miss Shinyanga 2014 bi Nicole Franklyn Sarakikya
kutoka wilaya ya Kishapu.Katika mashindano hayo ya kupata mrembo wa mkoa
wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Asela Promotions,mshindi wa kwanza
ameibuka na kitita cha Shilingi la 500,000/= na Laptop moja,mshindi wa
pili shilingi 350,000/= mshindi wa tatu shilingi 250,000/=,mshindi wa 4
shilingi 150,000/= na mshindi wa tano shilingi 150,000/= huku washiriki
wengine waliosalia kati ya 20 wakipata shilingi 100,000/= kila mmoja.
Msanii Mo Music akifanya yake jukwaani |
Kabla ya washindi kutangazwa majaji wakifuatilia kwa makini kilichokuwa kinajiri katika ukumbi wa NSSF mjini Kahama.Katikati
ni chief judge Flora Lauo kutoka Mwanza,kushoto ni bi Aneth Dotto
kutoka Arusha Miss Shinyanga mwaka 2003,kulia ni jaji Lutufyo Kanyenye
Kulia
ni bi Asela Magaka ambaye ni mkurugenzi wa Asela Promotions waandaaji
wa mashindano ya Miss Shinyanga 2014,wa pili kutoka kulia ni mkuu wa
wilaya ya Kahama ndugu Benson Mpesya,wa tatu ni naibu waziri wa
kilimo,chakula na ushirika Godfrey Zambi wakifuatilia shindano la Miss
Shinyanga 2014.
Waandishi
wa habari kutoka Kahama fm hawakuwa nyuma kushuhudia nani ataibuka
mshindi katika shindano la mrembo wa mkoa wa Shinyanga
Washiriki 20 wa shindano la Miss Shinyanga 2014 wakitoa show ya ufunguzi
Burudani
kutoka kwa mwimbaji wa taarabu nchini Mzee Yusuph ikiendelea,wakazi wa
Kahama na wananchi mbalimbali kutoka nje ya mkoa wa Shinyanga walipandwa
na mzuka na kuamua kucheza
Mshiriki wa Shindano
la kutafuta mrembo mwenye kipaji (Miss Talent Shinyanga 2014)
lililofanyika mjini Shinyanga Juni 25,2014 katika ukumbi wa NSSF,Irene
Makwaiya kutoka wilaya ya Kishapu akionesha kipaji chake cha kuimba
katika ukumbi wa NSSF mjini Kahama
Kazi haikuishia kumpata mrembo wa mkoa wa Shinyanga.Jukwaani ni Asela
Magaka ambaye ni mkurugenzi wa Asela Promotions waandaaji wa mashindano
ya Miss Shinyanga 2014 akimtangaza mshindi wa Shindano la kutafuta
mrembo mwenye kipaji(Miss Talent Shinyanga 2014) lililofanyika mjini
Shinyanga Juni 25,2014 katika ukumbi wa NSSF ambapo warembo 5 bora
walipatikana na jana mshindi alitangazwa ambaye ni Irene Makwaia kutoka
Kishapu
Miss Talent Shinyanga 2014 Irene Makwaiya kutoka wilaya ya Kishapu aliyeibuka na kitita cha shilingi 300,000/=
No comments:
Post a Comment