Saturday, July 11, 2015

TEAM LOWASA HAIJAKUBALIANA NA MATOKEO,..KUZUA VURUGU DODOMA LEO

VURUGU zimezuka mchana wa leo zilizodumu hadi majira ya alasili wakati kiza kikiingia wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea na mkutano wake.
Kutangazwa kwa majina matano na kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa (CC-NEC) ya chama hicho jana usiku, kumeibua mgawanyiko miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo, ambapo watatu wa wajumbe 32 wa kamati hiyo waliibuka wazi na kupinga uteuzi wa majina hayo mbele ya vyombo vya habari. 

 Baadhi ya Wanachama kwa idadi kubwa wameonekana waziwazi wakiandamana kuishinikiza Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM kulirudisha jina la mgombea wao Mhe. Lowassa.


Barabara kuu iendayo jengo kuu la Chama cha Mapinduzi mkoani (CCM) Dodoma, (Nyerere road) imegeuka kuwa ukumbi wa mkutano kwa umati wa watu kufurika.

Alasiri hii halmashauri kuu ya chama hicho ilifaanya kikao chake kupata majina matatu, halafu baadae leo jioni mkutano mkuu wa chama hicho unatarajiwa kukaa kupigia kura jina moja kati ya hayo matatu.
Yule atakayeibuka mshindi kati ya watatu hao ndiye atakaye kuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
                                                                  Askari kuingilia kati.
Polisi wakifanya kazi yao ya kutuliza gasia na kuwanasa wachache waanzilishi wa vurugu.
Tazama wanachama wemezagaa katika kila eneo la jumba hilo la mkutano Mjini Dodoma leo


Hii ndio taswila ya eneo ya jumba la mikutano ya CCM na maeneo jirani Mjini Dodoma.
djwillkan.blogspot.com

No comments:

Post a Comment