Timu ya Hekaheka imepokea taarifa zilizotokea hivi Punde kutoka Mwanza kuhusu hali ya sintofahamu kutoka kwa waumini wa kanisa la Baba God ambao wanaondolewa kwa amri ya mahakama baada ya kugoma kuondoka.
Kanisa linaitwa Cran of Glory linaloongozwa na baba Glory..waumuni hao walipewa eneo hilo kwa miaka mingi kwa ajili ya kusali wakati wakitafuta eneo lao lakini sasa wamegoma kuondoka wakidai mpaka Mungu wao awaambie.
Mwenye eneo akaamua kwenda kufungua kesi Mahakamani na Polisi walikuja na kuondoa baadhi ya vitu hivyo lakini wenyewe walivirudisha na wamewataka Polisi wasiguse madhabahu yao zaidi ya Mchungaji wao.
Pia kumetokea vurugu baada ya waumini kuanza kupiga kelele wakati Polisi wakitoa vitu.
Isikilize hapa mtu wangu…
No comments:
Post a Comment