Maafisa wa upelelezi wa ajali za ndege kutoka Misri wamesema kuwa
hawajapata ushahidi wowote kuwa ndege ya Urusi iliyoanguka katika rasi
ya Sinai na kuua watu 224 ililipuliwa.
Ndege hiyo iliyokuwa ikitokea Sharm el-Sheikh ikielekea Moscow ilianguka jangwani mwezi Oktoba.
Kundi moja la wapiganaji wanaoiunga mkono kundi la Islamic State (IS) walidai kuwa wao ndio walioidungua ndege hiyo.
Takriban watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo walikuwa ni raia wa Urusi.
Urusi yenyewe ilitangaza kuwa bomu iliyokuwa imetegwa ndani ya ndege hiyo ya Metrojet Airbus ndiyo iliyosababisha ajali hiyo.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na shirika la Urusi la kusimamia usafiri na
ajali za ndege ulipata chembechembe na mabaki ya bomu kwenye eneo la
tukio.
Urusi iliapa kuwaadhibu waliotekeleza shambulizi hilo.
Hata hivyo kiongozi wa wachunguzi kutoka Misri Ayman
al-Muqaddim,amenukuliwa na vyombo vya habari nchini humo akisema kuwa
''Hakukuwa na ushahidi wowote wa kuwepo kwa bomu ndani ya ndege hiyo
wala dalili za kitu chochote kilichoathiri usalama wa ndege hiyo.''
Wapiganaji wanaoiunga mkono Islamic State walisema waliiangusha ndege
hiyo ilikulipiza kisasi cha mashambulizi ya ndege za Urusi nchini Syria.
CHANZO CHA HABARI NA,..bbcswahili.com
LIKE PAGE: DJWillkan.com
No comments:
Post a Comment