Mkurugenzi wa 102.5 Lake FM, Doreen Estazia Noni akiiunua mfuko wa takataka na mtangazaji wa a kituo hicho Tatu Rajab wakati wa zoezi la kusafisha jiji la Mwanza lijulikanalo kwa jina la Ng'arisha Nzengo, Uchafu Nuksi. Zoezi hilo litakuwa linafanyika mara kwa mara.
Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishiriki katika kampeni ya 'Ng'arisha Nzengo'.
Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishiriki katika kampeni ya 'Ng'arisha Nzengo'.
Katibu wa wenyeviti wa mitaa jiji la Mwanza, Hamza Shido akishiriki katika kampeni hiyo ya 'Ng'arisha Nzengo' iliyoanzishwa na kituo cha redio cha 102.
Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishiriki katika kampeni ya 'Ng'arisha Nzengo'.
Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishangilia mara baada ya kuhitimisha kampeni ya kusafisha jiji la Mwanza ijulikanayo kwa jina la 'Ng'arisha Nzengo'.
Kituo
cha Redio cha 102.5 Lake FM kimezindua kampeni ya kufanya usafi kwa
jijini la Mwanza ijulikanayo kwa jina la Ng’arisha Nzengo, Uchafu Nuksi
yenye lengo la kuufanya mji huo kuwa msafi zaidi.
Mkurugenzi
wa kituo hicho Doreen Estazia Noni amesema kuwa wameamua kuanzisha
kampeni hiyo ya usafi ili kuupendezesha zaidi mji huo ambao ni minongoni
mwa miji mikubwa hapa nchini.Doreen amesema kuwa moja kati ya
vipaumbele vya kampuni ya Lake Fm nikuhakikisha inatoa mianya ya
kuiwezesha jamii kufikia kusudi la maendeleo binafsi na jamii nzima kwa
ujumla.
“Neno
ni la kabila ya Wasukuma lenye maana ya nyumbani, tumeamua kutumia neon
hili ili kufikisha ujumbe haraka kwa wakazi wa jiji la Mwanza, kampeni
hii ni endelevu kituo chetu cha redio kitaendelea kuhamasisha mpaka
kufikia lengo letu,”
“Kituo
chetu cha redio kimeamua kupanua wigo wake kwa kujihusisha katika
masuala mbalimabli ya kijamii na kutatua changamoto mbalimbali na kuleta
mtazamo chanya na si kuhabarisha na kuburudisha tu, naomba
ushirikiano mkubwa kwa wadau, serikali na watu binafsi katika
kufanikisha kampeni hii,” alisema Doreen.
Mbali
ya 102.5 Lake FM, kampeni hiyo pia imewashirikisha wadau wengine kama
Baamedas tv, Genic Studios , viongozi wa Jumuiya ya biashara ndogondogo,
minada na masoko , mwenyekiti Justin Sagala, mwenyekiti wa Afya
Minadani, Gosbert Lucas, katibu wa afya, Mariam Magembe, kiongozi wa wa
madereva wa daladala Dede Petro, serikali na Asasi binafsi.
Mkuu
wa maudhui na vipindi wa redio hiyo, Yusuph Magupa ambaye pia ni
mwenyekiti wa kampeni hiyo amesema kuwa afya ni ghali na wakazi wa
Mwanza wanapaswa kuishi katika mazingira salama ili kulinda afya yako.
Kupitia
uzinduzi wa kampeni hii iliyozinduliwa rasmi siku ya jumatatu ya Mei
Mosi, katika kipindi cha asubuhi cha Kokoliko, Magupa amebainisha mpango
mkakati wa kampeni hiyo kuwa nikuhakikisha elimu ya usafi kwa afya bora
inaeleweka na kuzingatiwa katika jamii.
Katibu
wa kampeni hii, Iman Hezroni ambaye ni pia ni mtangazaji wa redio hiyo
amesema kuwa mbali ya wao, kampeni pia imewashirikisha wakazi wa Mwanza
kwa asilimia kubwa ili kuzidi kujenga mahusihano mazuri baina ya kituo
na wananchi.
Hezron
amesema 102.5 Lake Fm itahakikisha inatoa fursa kwa wanajamii kusikika
na kueleza matakwa yao ili kutafuta mikakati ya matakwa yao kutafutiwa
ufumbuzi kwa kuwa kituo redio hiyo ipo kwa ajili wananchi.
Alisema
kuwa Mkurugenzi wa kampuni ya 102.5 Lake Fm kwa sasa anafanya
mazungumzo na Jumuiya ya biashara ndogo ndogo, minada na masoko ambapo
maazimio yaliyofikiwa ni kuijenga ziara maalum ya kuitembelea
minada yote ndani ya jiji la Mwanza, iliyopewa jina la Gulio la mtaa.
Alifafanua
kuwa dhamira ya ziara hiyo nikusogeza elimu ya usafi katika maeneo
hayo,uboreshaji wa huduma ya vyoo minadani pamoja na maboresho ya
kimiundombinu katika minada kupitia Gulio la mtaa lakini pia litatimiza
zana ya kupeleka radio kwa wananzengo, kwa kuhakikisha inawaburudisha na muziki wa kisasa pamoja na ule wa asilia.
CHANZO CHA HABARI: https://issamichuzi.blogspot.com
No comments:
Post a Comment