Monday, May 26, 2014

WASHIRIKI WAWILI WA MISS SHINYANGA CENTER 2014 WATOROKA KAMBINI USIKU WA KUAMKIA SIKU YA FINALI



Washiriki hawa wanaofahamika kwa majina yao (kulia ni Shakira Bryton, kushoto ni Witness Adam). Warembo hawa walitoroka usiku wa kuamkia ile siku ya kuchuana na warembo wenzao.

Sababu ya kutoroka warembo hawa inasemekana kua wenyewe hawakuja kwaajili ya kuchuana na mashindano ya urembo baali walikuja kibiashara zaidi.

Upande mwingine unaweza kuamini kweli walikua kibiashara zaidi, mtandao huu baada ya kumsogelea Mkurugenzi mwandaaji Elizabeth Steven(BETTY INTERTAINMENT) kweli alieleza baada ya kuwahoji washiriki wengine, waliowashuhudia wakati wa kijiandaa na kutoroka.

Waliondoka usiku mida ya saa 7:30, hata ivyo Mkurugenzi mwandaaji kwa upande mwingine alisema anashukuru sana kwani kati ya warembo wote kambini hawa walikua wanakiburi sana hawakua na heshima katika mazoezi hata wanapokuja Wazamini wao walikua ni watovu wa nizamu tu.

                                                 KIVIPI WALIKUA KIBIASHARA?
Kweli hata mimi naamini hivyo kwani hata tangu wamefika kambini nakumbuka walishawahi kulala kama wiki moja tu zingine zote walikua wakilala nje ya kambi. Kitu kingine ambacho kinanisikitisha wametapeli simu katika duka la simu la Sadiki ambalo liko Stand ya zamani, ni kitu cha aibu sana kwa mimi Mkurugenzi wa kampuni ya BETTY INTERTAINMENT, kwa sababu pia Sadiki naye ni miongoni kati ya Wazamini wangu.

No comments:

Post a Comment