Wednesday, July 23, 2014

AJALI YA BASI SUPER NAJIMNISA ILIYOTOKEA BUSANDA SHINYANGA NA KUJERUHI WATU 52

Basi la Super Najimunisa likiwa limeharibika vibaya baada ya kupata ajali jana Julai 22,2014 katika eneo la  Usanda-Samuye  mkoani Shinyang’a.basi hilo lililokuwa linasafiri kutoka Mwanza kuelekea Dar es salaam lilipinduka baada ya tairi zake za mbele kupasuka.
Wimbi la ajali za barabarani nchini Tanzania, limeendelea ambapo Abiria 63 waliokuwa wanasafiri kutoka Jijini Mwanza kwenda Dar es salaam na basi la Super Najimunisa lenye namba za usajili T.242 BRJ wamenusurika kufa baada ya basi hilo kupinduka katika kijiji cha Busanda kata ya Samuye wilaya ya Shinyanga mkoa wa Shinyanga jana Julai 22,2014, majira ya saa tatu asubuhi.

Basi hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina la Dickson Paulo.
Majeruhi 52 walikimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya matibabu.
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. Ntuli Kapologwe amewaambia wanahabari kuwa wamepokea majeruhi 52 ambapo kati yao majeruhi waliolazwa ni 22 na miongoni mwao ,wanne kati yao hali zao ni mbaya na tayari majeruhi 30 wamesharuhusiwa.
 Aidha Majeruhi waliolazwa katika hospitali hiyo wamesema ajali hiyo imetokea baada ya tairi la mbele la basi hilo kupasuka na gari kupinduka mtaroni
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, SACP Justus Kamugisha alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kwamba pamoja na kupasuka kwa tairi basi hilo lilikuwa katika mwendo kasi.
Kamanda Kamugisha amesema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo.

Basi la Super Najimunisa likiwa limeharibika vibaya baada ya tairi zake za mbele kupasuka .


Wataalamu wa Afya kutoka mkoa wa Shinyang'a wakitoa huduma ya tiba kwa wahanga wa ajali ya basi la Najmunisa katika eneo la tukio iliyotokea Julai 22,2014 Asubuhi.

Vilio vilitawala,majeruhi wakiwa taabani baada ya kupata maumivu sehemu mbalimbali za mili yao na hapa wanapatiwa matibabu.

Kaimu mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga lnsp Vicent Msami akikagua basi hilo katika eneo la tukio, ambapo alisema ajali hiyo pia imechangiwa na mwendo kasi.

Basi la Super Najimunisa likiwa eneo la tukio jana Julai 22,2014 huku abiria wakihangaika baada ya ajali hiyo ambayo imejeruhi watu 52 kati 63 waliokuwa ndani ya basi hilo.


Huduma kwa majeruhi zikiendelea ambapo imeelezwa kuwa majeruhi waliolazwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ni 22,kati yao wanaume ni 13 na wanawake 9.



Habari moto moto na djwillkan.com

No comments:

Post a Comment