|
Hapa
ni ndani ya ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,ambako leo
kumefanyika mkutano mkuu wa mwaka wa halmashauri ya manispaa ya
Shinyanga.Mambo kadha wa kadha yamejadiliwa,lakini pia uchaguzi wa
kumpata naibu meya kwa awamu ijayo ya mwaka 2014/2015 umefanyika.Kushoto
ni diwani wa viti maalum kupitia CHADEMA bi Zainabu Heri,kulia kwake ni
mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA mheshimiwa Rachel Mashishanga
wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika mkutano huo/Baraza la madiwani
wa manispaa ya Shinyanga yenye kata 17
Aliyesimama
ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga(mwaka 2013/2014) ndugu David
Nkulila,diwani wa kata ya Ndembezi kupitia ccm akizungumza kabla ya
kufanyika kwa uchaguzi wa nafasi ya naibu meya mwaka 2014/2015.Kushoto
kwake ni mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga ndugu Gulam Hafeez
Mukadam,kulia ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Dkt Anselm Tarimo |
|
Baraza
la madiwani linaendelea ndani ya ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa
Shinyanga leo,ambapo uchaguzi kiti cha naibu meya ambaye kisheria
kufanyika kila mwaka umefanyika |
|
Waandishi wa habari nao walikuwepo,pichani kila mmoja yuko bize kivyake |
|
Katika
baraza hilo la madiwani wa manispaa ya Shinyanga wajumbe wa kamati
mbalimbali walitangazwa,kamati hizo ni pamoja na kamati ya
miundombinu,uchumi na elimu,Ukimwi,Ajira na kamati ya fedha Kushoto
ni mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga bwana Festo Kang'ombe
akizungumza jambo na mstahiki meya ndugu Gulam Hafeez Mukadam,wa tatu ni
mwenyekiti wa muda wakati wa uchaguzi wa naibu meya ndugu Thomas Chuma
Maganga diwani wa kata ya Lubaga kupitia chama cha mapinduzi |
Diwani wa kata ya Kitangiri kupitia
CHADEMA ndugu George Mussa Kitalama (aliyeteuliwa na chama kugombea
nafasi hiyo)akiomba kura kutoka kwa wajumbe 21 waliotakiwa kupiga kura
kuchagua naibu meya wa manispaa ya Shinyanga katika mwaka 2014/2015
|
Kulia
ni katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga ndugu Boniface Chambi,kushoto
kwake ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Dkt Anselm Tarimo
wakifuatilia uchaguzi wa nafasi ya naibu meya |
Diwani wa kata ya Ndembezi kupitia ccm
ndugu David Nkulila,ambaye aliteuliwa na ccm kugombea kiti cha naibu
meya akitetea kiti chake/akiomba kura kwa wajumbe ili wampatie ridhaa ya
kuwa naibu meya tena wa manispaa ya Shinyanga kwa mwaka
2014/2015.Nkulila alikuwa naibu meya mwaka 2013/2014 lakini kutokana na
chama chake kumwamini kwa uchapakazi wake wamemteua kuwania kiti hicho
katika mwaka 2014/2015
|
Kampeni
kutoka kwa wagombea kutoka vyama viwili yaani CCM na CHADEMA
zinaendelea.Baraza la madiwani wa manispaa ya Shinyanga linaundwa na
madiwani kutoka vyama viwili pekee vya upinzani |
|
Ndani ya ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo madiwani wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea |
|
Zoezi
la kukusanya kura linaendelea,afisa habari wa manispaa ya Shinyanga
ndugu Gaudiozi Mwombeki akikusanya kura,hapa ni katika awamu ya kwanza
ya uchaguzi ambayo iliingiwa dosari baada ya baadhi ya wajumbe kukusanya
kura zao kwa pamoja,hali ambayo ililalamikiwa na wajumbe wengine kwani
ilikuwa na harufu ya uchakachuaji wa kura.Awamu ya pili(marudio) kila
mjumbe alipiga kura peke yake na hatimaye mshindi akapatikana |
|
Tunasubiri matokeo yatangazwe........ |
|
Kufuatia
uchaguzi huo wa kiti cha naibu meya,mshindi alitangazwa David Mathew
Nkulila,diwani wa ccm kata ya Ndembezi,aliyekuwa anatetea kiti
hicho,ambapo alipata kura 15,huku mgombea mwenza,George Mussa
Kitalama(CHADEMA) akipata kura 6 |
Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga kwa awamu ya tatu sasa ndugu David
Mathew Nkulila akizungumza baada ya ushindi wa kishindo ambapo
aliwataka madiwani na wataalamu kuwajibika kama inavyotakiwa katika
kuwaletea maendeleo wananchi,huku akiomba ushirikiano kwa madiwani na
wataalam hao katika kuhakikisha kuwa ilani ya ccm inatekelezwa kama
inavyotakiwa.
Naibu meya huyo alitumia fursa hiyo
kuwataka watendaji/wataalam kutekeleza maazimio ya vikao vya baraza la
madiwani kwa wakati unaotakiwa huku akisisitiza kuwa hataki kuona
ufisadi wa aina yoyote katika manispaa hiyo
Habari moto moto na djwillkan.com
No comments:
Post a Comment