Leonardo
DiCaprio alipiga picha na Mandela wakati alipokuwa aki shoot movie
"Blood Diamond" South Africa na mandela aliiandika picha hiyo "To Leo DiCaprio, Best Wishes, Mandela, 4-8-07."
cha ajabu picha hiyo haikuwahi kumfikia Leo, watu wa karibu na muigizaji huyo waliiambia TMZ na Leo anaamini kuwa iliibiwa.
thamani ya picha hiyo mwisho wa siku iliifikia kampuni moja inayoitwa "Moments in Time",ambayo kwa sasa inaiuza picha hiyo kwa $25,000.
Leo
anataka picha hiyo irudishwe na kwa mujibu wa NY Post ameongea na
mwanasheria wake juu ya kampuni hiyo, lakini Moment in Time inamwambia
Leo kuachana nao kwasababu wana haki zote juu ya picha hiyo.
Kama ulikuwa hujui kuna kitu komoja katika sheria kinachoitwa "bona
fide purchaser," ikiwa na maana yakuwa kama mtu amenunua kitu bila ya
kujua kuwa ilipatikana pasipo kihalali, mtu huyo ana haki zote za
kumiliki kitu hicho kwa vyovyote vile.
mmiliki wa kampuni hiyo, Gary
Zimet,ameiambia TMZ kuwa alinunua picha hiyo ndani ya mwezi uliopita na
anategemea kuiuza katika siku chache zijazo. Zimet amesema hahusiki kwa
lolote kuhusuiana na madai ya Leo.
No comments:
Post a Comment