Stars wanataraji kupambana na Mozambique na kama ilivyotarajiwa Nadir Haroub na John Bocco kusababisha ziara hiyo.
Shomari Kapombe, Mrisho Ngasa and Kelvin Yondani ni wachezaji wengine muhimu katika kikosi cha Nooij chenye wachezaji 26 ambacho kimewajumuisha pia Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Ramadhan Singano, Said Morad na Ramadhan Singano.
Akizungumza kwa niaba ya Nooij,kocha msaidizi,Salum Mayanga alisema kuwa wachezaji wangejumuika pamoja siku ya Jumatatu kabla ya kuelekea Gaborone nchini Botswana kwaajili ya kuweka kambi ya muda.
Stars ambao wameingia kwenye raundi ya pili ya kuwania kufuzu kwa michuano ya mataifa ya Afrika 2015 mara baada ya kuishinda Zimbabwe mapema mwezi huu watacheza na Mambas(Mozambique) Julai 20 katika raundi ya kwanza ikiwa ni mchezo wa kwanza ambao utapigwa kwenye dimba la Taifa.
Wachezaji wengine katika kikosi cha Nooij ni Deogratias Munishi, Aishi Manula, Benedicto Tinoko, Joram Nason, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris, Pato Ngonyani, Frank Domayo, Jonas Mkude na Saidi Juma.
No comments:
Post a Comment