Hapakuwa na kiingilio,African Barrick waliwezesha mpanga mzima-Pichani
ni Wakazi wa Kahama wakiwa katika uwanja wa taifa usiku wa kuamkia leo
wakati mechi ya fainali kati ya Argentina na Ujerumani zikiumana vikali
nchini Brazili.Wakazi hao wa Kahama mbali na Kushuhudia mechi za kombe
la dunia pia walipata fursa ya kupata burudani kutoka kwa wasanii
mbalimbali akiwemo Ney wa Mitego,Christaina Bella na wasanii kutoka
Kahama
Msanii Ney wa Mitego akiwakuna wakazi wa
Kahama usiku wa kuamkia leo mjini Kahama,African Barrick Gold ndiyo
waliofadhili mpango mzima,ikiwa ni katika kuimarisha uhusiano wao na
jamii inayowazunguka,lakini kuonesha kuwa migodi ni kwa manufaa ya
wananchi
Wimbo wa Ney wa Mitego ukaibua hisia_Maisha menyewe mafupi.........
Ney anakamuaaaa_Burudani
kwa wakazi wa Kahama ilikuja muda mfupi baada ya kumalizika kwa Soka
Bonanza ambapo jumla ya timu 8 za mpira wa miguu kutoka Kahama zilikuwa
zinashiriki mashindano hayo.Mshindi wa kwanza alikuwa Bodaboda
fc,akifuatiwa na Afya fc ambao waliingia fainali kama ilivyokuwa katika
kombe la Dunia Argentina na Ujerumani huko Brazil
Ebwana eee,ilikuwa burudani sana,hayo
yote ni kwa sababu ya uwepo wa kampuni ya uchimbaji madini ya African
Barrick Gold inayomiliki mgodi wa Buzwagi na Bulyanhulu wilayani
Kahama,lakini Brazuka Bonanza mjini Kahama ilikuwa inasimamiwa na mgodi
wa Buzwagi
Mwenye nguo nyeupe ni msanii matata
kutoka Kahama anajulikana kwa jina la Joslin Abraham akichana mistari
mbele ya Ney wa Mitego.Mbali na msanii huyo kutoka Kahama kuonesha
kipaji chake cha kuimba pia wasanii wengi wa Kahama walipanda jukwaani
na kufanya mambo makubwa,hakika ilikuwa full shangwe,tena bila
pesa,wengi wakisema "Asante Buzwagi"
Msanii Christian Bella akishambulia
jukwaa katika uwanja wa taifa Kahama usiku wa kuamkia leo ambapo maelfu
ya wakazi wa Kahama walikuwepo katika uwanja huo
Msanii Christian
Bella akifanya yake mjini Kahama.Mbali na kupata burudani kutoka kwa
wasanii mbalimbali walioletwa na African Barrick,wakazi wa Kahama
walishuhudia live mechi ngumu kati ya Argentina na Ujerumani,hakuna
aliyelala mpaka kikaeleweka Ujerumani 1,Argentina 0.
No comments:
Post a Comment