Friday, August 22, 2014

WEUPE PYEEE WAJA NA VIDEO MPYA YA UJIO-___-SOON UTAIONA

Hii ni baada ya kutoka na HUNDERE, sasa ni Video mpya ya WEUPE PYEEE inayoitwa UJIO wamemshirikisha YUZO kutoka EAST COAST TEAM. Ukweli ni kwamba vijana hawa wanakuja juu sana katika game hii ya muziki wa bongo flavour, kati ya wakali wote wa kanda ya Ziwa hawa ni nooouma CELLO B, MAFIA THE INC pamoja na NKUNDA STAR.

Wanazidi kufanya vizuri kutokana na ushirikiano mkubwa kabisa wa KAMPUNI YA WEUPE PYEEE hasa wanapokuwa katika  kazi zao za muziki ni ushirikiano wa dhati ambao kila mmoja wa Weupe anakuwa makini kulingana na kitengo chake.Dj Willkan ni mmoja wa kundi hilo katika kusimamia kila kitu kinakwenda sawa hasa katika upande wa Nkunda Star, Mafia pamoja na Cello B wanapokuwa jukwaani wakifanya yao Dj Willkan kama kawaida katika upande wa moja na mbili mpaka mwisho wa show. Vile vile katika upande wa kupendeza wakati wa kufanya shooting ama wakiwa tayali kwa show, Swala zima la make up hapo pia utakutana na kinadada makini sana BEATRIC pamoja na J-PHRIDER. Hii ndio kampuni nzima ya Weupe Pyeee.


                                                                    djwillkan.blogspot.com

No comments:

Post a Comment