Friday, September 26, 2014

CASH Kings 2014; FORBES Watoa List ya wasanii wa hip hop Duniani wanaolipwa mkwanja mrefu

Mwanzoni mwa mwaka huu Apple walimwaga dola biliono 3 kuinunua Beats, kampuni ilianzishwa na Dr Dre na Jimmy Lovin, Ingawa ilikuwa ni haraka sana kudai kuwa msanii wa kwanza bilionea wa hiphop (kitu ambacho hakiwezi kutoa sasa hivi) lakini Dre yuko njiani kuelekea huku 
Kwa hivi sasa Dre amewatupa mbali wasanii kibao juu ya mafanikio ya kifedha ambapo ndani ya miezi 12 iliyopita ameingiza dola milioni 620 (bila makato). Kiwango hicho cha fedha sio tu kuwa ni kiwango kikubwa sana kuingiza ndani ya mwaka kwa msanii (kilichowahi kuripotiwa na forbes) bali ni ni zaidi ya kuchanganya mapato ya wasanii 24 wanaomfata nyuma katika list ya wasanii wa hiphop wenye mkwanja 2014
Nafasi ya pili imekatwa na Didiy na Jay Z ambao wamefungana, wote wakiwa wameingiza dola milioni 60, kama unakumbuka didy alikuwa nafasi ya kwanza mwaka jana na Dre alikuwa nafasi ya 3.
nafasi ya nne imeshikiliwa na Drake ambaye ameingiza dola milioni 33, yakiwa ni mapato kutokana na album yake ya nne Nothing Was the Same, ambayo imeuza kama copy millioni 4 duniani kote huku mkwanja mwingine ukiwa umetokana na tour ya Arena na endorsement deal ya Nike "Jordan" zimempeleka kuongeza kipato mara tatau ya mwaka jana alipokuwa na kipato cha dola milioni 10.5

wengine katika list hiyo nipamoja na

5. Macklemore & Ryan Lewis -  $32 million. 
 
6. Kanye West: $30 million
7. Birdman: $24 million
8. Lil Wayne: $23 million
9. Pharrell Williams: $22 million 

10. Eminem: $18 million
11. Nicki Minaj: $14 million
12. Wiz Khalifa: $13 million
13. Pitbull: $12 million
14. Snoop Dogg: $10 million 
15. Kendrick Lamar: $9 million

16. Ludacris: $8 million (tie)

16. Tech N9ne: $8 million (tie)

16. Swizz Beatz: $8 million (tie)

16. 50 Cent: $8 million (tie)

20. Rick Ross: $7 million (tie)

20. J. Cole: $7 million (tie)

20. DJ Khaled: $7 million (tie)

20. Lil Jon: $7 million (tie)

 

djwillkan.blogspot.com

No comments:

Post a Comment