Picha lilianza ivi |
Hellen George mshindi wa Serengeti Fiesta Super Nyota 2014 katika picha ya pamoja na majaji |
Mashindano ambayo yalikusanya jumla ya wasichana 14 kutoka miji 14
tofauti kwa ajili ya kutafuta kipaji kimoja ambacho kitawakilisha hiyo
miji mingine hatimaye kimepatikana usiku wa kuamkia October 18 pale
Escape 1.
Meza ya majaji 4 wakiongozwa na Dj Fetty walikua na kazi ya
kuhakikisha wanapata kipaji kimoja ambacho mbali na kupewa zawadi ya
Milion 1 taslim pia atapata nafasi ya kupiga colabo na Diamond Platnumz
na darasa la muziki kutoka kwa Barnaba.
Hellen George ndiye aliyepata nafasi hii kwa kuibuka mshindi wa
mashindano haya kwa mwaka huu ambaye anawakilisha mkoa wa Dar es
salaam,mara baada ya kutangazwa mshindi,millardayo.com ilipata nafasi ya kufanya nae interview fupi juu ya ushindi huo.
Namshukuru Mungu kwa hii nafasi na nafurahi kwa kamati iliyoandaa
shindano hili kwani imelenga kuinua vipaji vyetu,kiukweli shindano
lilikua gumu na lilikua linahitaji moyo,nimejisikia furaha kutangazwa
mshindi’
‘Mshiriki niliyekuwa namuangalia zaidi ni mshiriki kutoka Mwanza sio
kwamba nilikuwa namhofia lakini nilimgundua ana kitu tofauti kwenye
sauti yake,nafasi hii nimeifurahia kwa sababu Diamond Platnumz ni msanii
ambaye nampenda sana,nilishawahi rekodi single 1 mpaka sasa lakini
haikwenda radio’-Hellen George.
djwillkan.blogspot.com
No comments:
Post a Comment