Rapper Jay Z na mke wake wapo Paris Ufaransa wiki hii ambapo wakati
Jay akiwa kwenye matembezi huku akiwa amembeba mtoto wake ilitokea mmoja
wa Watalii baada ya kumuona Jay akauliza ‘huyu ni nani? unajua jibu
alilotoa mume huyu wa Beyonce?
Kabla ya Jay Z kujibu, mlinzi wake aliekua ametangulia mbele hatua chache huku Jay akifata kwa nyuma na timu yake alikua akizuia watu kupiga video ambapo huyu mtalii alikua akipiga video, akawa anashangaa imekuaje akatazwe kupiga video… swali lililoambatana na kuuliza huyu anaepita nani? Jay Z kwa kiburi na yeye akamjibu kwa kuuliza ‘wewe ni nani?‘
Japo inaonekana Jay Z alijibu kwa dharau, wataalamu wa mambo wanasema huenda kweli mtalii huyu hakuwa anajua anaepita ni nani manake alikua kwenye eneo la kitalii ambalo wengi wanaokuwepo hapo huchukua kumbukumbu kupitia camera zao.
No comments:
Post a Comment