Elizabeth Michael maarufu kama LULU, muigizaji wa Films (Bongo Movie). Ni muigizaji anayelipwa pesa nyingi kuliko yeyote hapa nchini. Na hii ni kutokana na kujitambua na kuelewa nini anachotakiwa kufanya katika tasnia nzima ya Filam. Kujithamini na kuthamini kile ambacho unajua kinakuletea ugali ni jambo la msingi sana, na huu ni mfano mzuri wa kuigwa kwa waigizaji wengine. Kwa sasa ukimuhitaji LULU kwenye filam yako nje na Kampuni yake ya PROIN PROMOTIONS ghalama ya chini ni Sh million 15!!??...na hii ni punguzo tofauti na ile utakapomchukua ndani ya Kampuni. Wasanii wengine wa Bongo Movie wanajirahisi sana katika swala la bei wengine mpaka kuanzia laki nane hadi million wanachukua, lakini nao wakigundua na kuthamini kazi zao kama LULU naamini kabisa tutafika mbali.
Hii ni Challenge kubwa sana kwa wasanii wa Bongo Movie, wapatikane wengine kama 10 hii atasaidia hata kwa Mwananchi kununua kazi kwa bei ambayo ata yeye atalizikanayo kwani hata ubora wa kazi kwa watemgenezaji ama Shooters watakuwa makini kwa sababu watakuwa wakijua dhahili hela iliyotoka ni ndefu, hivyo kutatoweka kabisa ulipuaji wa kazi za Wasanii.
No comments:
Post a Comment