Friday, March 6, 2015

Tamasha la Chakula cha Kiafrika kufanyika Jumapili hii Jijini Arusha

Tamasha hili la Chakula cha Kiafrika litafanyika katika Mgahawa wa Umbrella (Umbrella Garden and Restaurant).

Akizungumzia tamasha hilo, Elihuruma Msengi alisema lengo la kufanya tamasha la Chakula cha Kiafrika ni kuwakumbusha Watanzania umuhimu wa lishe na chakula cha Kiafrika kwani magonjwa mengi yanatokana na vyakula vya Viwandani na pia kudumisha upendo na amani wa Jiji la Arusha.

Ameongezea kwa siku hiyo ya jumapili itakuwa ni siku ya Wanawake Duniani hivyo tamasha litawapa elimu wanawake ya lishe kwasababu wao ndio wahusika wakuu.

Wasanii wa Bongo Fleva wa kundi la Navy Kenzo, Aika na Nahreel watahusika kutoa elimu ya lishe ya Chakula cha Kiafrika.

Wengine watakaohudhulia tamasha ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Afisa Tawala wa Mkoa, Ofisi ya Afya na Madiwani baadhi wa Mkoa huo.

Kiingilio ni Sh 15 kwa watu wazima na watoto wawili wanafunzi watalipa Sh 7500 wakiwa na vitambulisho. Tamasha litaanza saa 6 mchana hadi saa kumi na mbili jioni.

No comments:

Post a Comment