Lile bifu lililokuwa likiwaweka umbali wa kutokusalimiana wala kusogeleana kati ya Matonya na Tunda Man limefikia mwisho leo. Hii ni baada ya Tunda Man kualikwa kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds fm, ndipo walizungumzia mengi kuhusu ugomvi wao yeye na Matonya.
Tunda Man alikili kuwa kweli kuna makosa na anaomba msamaha kwa Matonya. Ndipo ilipofanyika saplaizi kwa Tunda baada ya kuitwa Matonya kwenye Leo Tena pasipo kufahamu chochote kama Matonya ameitwa ili waje wayamalize live ndani ya Clouds Fm.
Kiukweli Matonya alipowasili alidai kwamba Tunda ni mdogo wake, kiroho safi amemsamehe. Waliyamaliza kiume na mwisho kabisa Matonya alisema baada ya kutoka ndani ya Clouds moja kwa moja na mdogo wake Tunda mpaka Studio kwajili ya kufanya collaboration.
Mpenzi msomaji wa djwillkan.blogspot.com endelea kutembelea blog hii itakufahamisha kuhusiana na nyimbo hiyo itakapokuwa tayali.
No comments:
Post a Comment