Black Ryno amesema baada ya kumaliza masters yake MZUMBE sasa
akili yake imekua na ataachia albamu yake muda si mrefu kwani sasa
anajua nini anafanya ili kazi zake ziweze kuuzika na kumpatia faida
zaidi…jamaa pia kasema atakua anauza kazi zake kupitia mitandao ya
kijamii na kwenye Supermarkets kubwa ili zimfikie kila mmoja tofauti na zamani.
Kingine kilichosikika leo kwenye 255 ni kumhusu Nay wa Mitego ambaye amefunguka na kusema hakuwa amepanga kutoa single yake ya ‘Sina muda’ bali mashabiki ndio waliomlazimisha kwa sababu bado ‘Mapenzi au Pesa’ ilikua ikifanya vizuri.
Amesema video zote zitatoka wakati wowote kuanza sasa.
DX kutoka Noise Maker kutoka Arusha amesema anamuelewa sana mtayarishaji chipukizi Mens Selector
kutokana na uwezo wake mkubwa..amekua akitayarisha nyimbo wakati huo
huo ni mwanamuziki….ana ubunifu mkubwa kwenye kazi yake kwa sababu yuko
sehemu tofautitofauti.
No comments:
Post a Comment