|
Meneja
wa Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Estelina Sanga maarufu kwa jina
la “Linah”, Doreen Noni toka Kampuni ya Panamusiq inayosimamia kazi za
msanii huyo (wa kwanza kulia) akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo
Pichani) kuhusu udhamini wa video ya msanii wake walioupata toka Kampuni
ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Jebel na kufafanua zaidi
juu ya uzinduzi wa video hiyo mpya itakayotambulika kwa jina la “No
Stress” anayotarajia kuzindua hivi karibuni. Wa pili kulia ni msanii
Linah na wa tatu ni Meneja chapa wa pombe kali SBL, Shomari Shija na
kushoto ni Meneja uvumbuzi SBL , Attu Mynah. Hafla hiyo imefanyika makao
makuu ya kampuni hiyo Chang’ombe jijini Dar es Salaam. |
|
Msanii
maarufu wa Muziki wa kizazi kipya, Estelina Sanga maarufu kama “Linah”
(wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo
pichani juu ya Video yake mpya ijulikanayo kama” No Stress”
inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni chini ya udhamini wa Kampuni ya
bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Jebel Coconut, katikati ni
Meneja chapa pombe kali toka SBL, Shomari Shija na Meneja uvumbuzi SBL,
Attu Mynah. Tukio hilo limefanyika makao makuu ya kampuni hiyo
Chang’ombe jijini Dar es Salaam. |
|
Meneja
chapa wa pombe kali SBL, Shomari Shija (katikati) akiongea na waandishi
wa habari (hawapo pichani) juu ya udhamini wa uzinduzi wa video mpya ya
msanii Estelina Sanga “Linah” itakayokwenda kwa jina la “No Stress”
kupitia kinywaji chake cha Jebel Coconut. Kushoto ni Meneja uvumbuzi
SBL, Attu Mynah, na kulia ni msanii Linah. Tukio hilo lilifanyika makao
makuu ya SBL Chang’ombe jijini Dar es Salaam. |
|
Meneja
uvumbuzi SBL, Attu Mynah, (kushoto) akiongea na waandishi wa habari
hawapo pichani kuhusu udhamini wa video mpya ya msanii “Linah” kupitia
chapa ya Jebel coconut toka SBL chapa ambayo msanii huyo ni balozi.
Video hiyo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni na itakwenda kwa jina
la “No Stress” (Wa pili) ni msanii Linah na wa kwanza kulia ni Meneja wa
msanii huyo Doreen Noni toka kampuni ya Panamusiq inayosimamia kazi za
msanii huyo. (Wa pili) kushoto ni Meneja chapa pombe kali toka SBL,
Shomari Shija. |
|
Meneja
chapa pombe kali toka SBL, Shomari Shija (kushoto) akiongea na
waandishi wa habari hawapo pichani juu ya udhamini wa uzinduzi wa video
mpya ya msanii maarufu Estelina Sanga a.k.a Linah” (katikati)
itakayojulikana kwa jina la “No Stress”. Udhamnini wa msanii huyo
unafuatia ahadi ya Kampuni ya bia ya Serengeti kusapoti kazi zake baada
ya msanii huyo kupata mkataba wa ubalozi wa kinywaji cha Jebel Coconut
toka SBL. (Kushoto) ni Meneja wa msanii huyo Doreen Noni toka Kampuni ya
Panamusiq inayosimamia kazi za msanii huyo. Tukio hilo lilifanyika
makao makuu ya SBL Chang’ombe jijini Dar es Salaam. |
KAMPUNI
ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Jebel Coconut imetangaza
rasmi siku ya leo dhamira yake ya kudhamini uzinduzi wa video mpya ya
msanii Estelinah Sanga maarufu kwa jina la kisanii “Linah” itakayo
kwenda kwa jina la “No Stress”.
Video ya wimbo huo imefanyika nchini
Kenya na Afrika ya kusini ambapo kwa kushirikiana na menejimenti ya
msanii huyo, SBL imeweza kudhamini utengenezaji wa video hiyo ambayo
hadi sasa imeshakamilika huku Kampuni hiyo ikisubiria kuizindua rasmi
kwa wananchi.
Hatua ya SBL kudhamini video ya
wimbo huo ni njia mojawapo ya Kampuni hiyo kutambua sanaa ya muziki hapa
nchini ambapo pia hapo awali Kampuni hiyo iliahidi kumsapoti msanii
huyo mara baada ya kupata mkataba wa mwaka mmoja wa kuwa balozi wa
kinywaji cha Kampuni hiyo cha Jebel coconut.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa utoaji wa taarifa hiyo kwa
umma, Meneja Uvumbuzi wa kampuni hiyo Attu Mynah alisema “Kampuni ya bia
ya Serengeti inatambua umuhimu wa Sanaa ya muziki hapa nchini na siku
zote inalenga kumuwezesha msanii aweze kufikia malengo ya ndoto zake.
Tumeamua kudhamini utengenezaji na uzinduzi wa video ya wimbo wa msanii
Linah kwa kuwa tunatambua uwezo wake na tungependa afike mbali zaidi
kimuziki”.
, alisema “Tunafuraha kwa kuwa
Kinywaji chetu cha Jebel coconut kinaendelea kujizolea mashabiki wengi
kupitia ubalozi wake ambapo ameendelea kuitangaza chapa hii sehemu
mbalimbali za Tanzania. Kama SBL tunajivunia kudhamini baadhi ya kazi
zake na ni matumaini yetu kuwa kupitia udhamini huu ataendelea kufanya
vizuri zaidi katika ngazi za kimataifa”.
Jebel
coconut ni aina ya pombe kali yenye ujazo wa 250ml inayotengenezwa
nchini Tanzania na Kampuni ya bia ya Serengeti ambayo imebuniwa na
kutengenezwa kwa ladha ya nazi ambazo zinapatikana kwa wingi hapa
nchini. Jebel pia ni kati ya pombe kali zaidi ya 10 za kimataifa
zinazosambazwa na kampuni ya bia ya Serengeti huku walengwa wa kinywaji
hiki wakiwa ni watu wazima na wenye umri wa kati.
No comments:
Post a Comment