Tuesday, July 7, 2015

YEMI ALADE AZUNGUMZIA SABABU YA KUWASHAMBULIA WANDAAJI WA TUZO ZA BET


BAADA ya mwimbaji maarufu wa Nigeria, Yemi Alade, maarufu kama  Jonny Crooner kutokana na wimbo wake, kushindwa katika mpambano wa Tuzo za BET nchini Marekani, amewashambulia waandaji wa mashindano hayo kwamba hawakuwafanyia haki waimbaji kutoka Afrika.


“Kusema ukweli Waafrika hatutendewi haki kama wenzetu kutoka mabara mengine,” alisema mwimbaji huyo mrembo akisisitiza kwamba hakusema hivyo kwa vile hakupata tuzo yoyote kwenye mashindano hayo.

Aliongeza kwamba iwapo atachaguliwa tena kushiriki BET, hilo anamuachia Mungu ambaye ndiye Hubariki na si binadamu.  Iwapo Mungu ataendelea kunibariki, hakuna awezaye kulizuia jambo hilo.”


djwillkan.blogspot.com

No comments:

Post a Comment