Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) July 30 walimkabidhi barua ya kumsimamisha Shilole
kufanya kazi za muziki kwa muda wa mwaka mmoja,taarifa ambayo
iliwashtua wadau wengi wa muziki kuhoji zaidi kuhusu hukumu hiyo namna
ilivyofanywa.
Kama unakumbuka miezi 3 iliyopita Shilole alienda kufanya show nchini Ubelgiji
wakati akitumbuiza jukwaani kwa bahati mbaya sehemu ya kifua
chake(TITI) ilijitokeza kwa nje baadae picha zikapigwa na kusambaa
kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya hukumu hiyo millardayo.com
ilipata nafasi ya kuongea na Shilole ambapo aliuliza maswali manne kwa
Basata kama wasimamizi wa shughuli zote zinazohusu sanaa kwa Tanzania.
1.Kwanini barua imekuja baada ya kupost show yangu ya kwenda Marekani kufanya show?
2.Mmenifungia muziki wangu,Mnataka nikaishi wapi?na mnasema vijana tujiajiri,ajira niliyojiajiri ni hii mnataka nifanye ipi?
3.Nina familia ya watu 10 ndani kwangu,wote wananitegemea wengine
wanasoma Boarding,nina watoto yatima wengine wanasoma kupitia muziki huu
huu na ninalipa kodi ya nyumba,Mnataka Basata tufanye nini?
4.Ninahangaika,ninapambana na kazi zangu kwa nguvu zangu,Mnataka
nikajiuze nipate ukimwi?mnataka nikabebe Dawa za kulevya nikauwawe?kwa
sababu najituma kwa kazi yangu na nguvu yangu kama mnavyoona kwenye
jukwaa hata vitabu vya Mungu vinasema asiyefanya kazi na asile.
No comments:
Post a Comment