Huu ni msimu wa kumi na saba kwa TBL tangu waanzishe uzamini wa mashindano ya mbio za Baiskeli. Wakati huo bia iliyokuwa ikizamini mashindano haya ni Bia ya Safari Lager, ambayo imekuwa ikizamini michezo mingi ikiwemo POOL TABLE na SFARI NYAMA CHOMA. Kwa msimu huu wa 17 Bia ambayo pia na yenyewe imekuwa ikizamini mashindano ya Mitumbwi pamoja na Ngoma za asili. Imejinyakulia sifa nyingi na kuwakutanisha watu pamoja hasa wakati wa kusherehekea mavuno, kwa msimu huu pia imezamini Mbio za Baiskeli, zinazotarajia kufanyika siku ya NANE NANE Mkoani Shinyanga.
Mashindano haya itakuwa kama ifuatavyo; Kwa Wanaume wataanzia SHINYANGA hadi KAHAMA na kurudi SHINYANGA Km=220, Wanawake pia wataanzia SHINYANGA hadi ISAKA na kurudi SHINYANGA Km=130. Pia kwa waremavu watazihesabu Km=12 kwa kuzunguka uwanja mara 30, pamoja na mbio za Baiskeli kwa wanawake huku wakiwa wamebeba ndoo kichwani kwa kuzunguka uwanja Km=4.
Pia kutakuwepo na mashindano ya BALIMI NYAMA CHOMA kwa Baa ambazo zitashiriki mashindano hayo ni MASAUNA BAA{Free Park A}, SHERATON, OSAKA BAA, UNIQUE PUB na LUBAGA INN BAA. Zawadi nono kutoka Tanzania Breweries Limited {TBL}.
No comments:
Post a Comment