Later
on Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha
kutokea kwa ajali hiyo ila alikanusha jina la Tunda Man kuwepo kwenye
idadi ya walijeruhiwa kwenye ajali hiyo na kuthibitisha kuwa ajali hiyo
ilisababisha kifo cha dereva wa gari lililopata ajali aliefahamika la
Musa Katuzo maarufu kama Man Katuzo.
Hata hivyo inaonekana kama Tunda Man alikua akitumia ajali hiyo kama
“Kiki” kama watoto wa mjini wanavyosema kwani,kupitia akaunti yake
Facebook,afisa uhusiano wa kituo cha redio cha Ebony Fm kituo ambacho
Tunda Man na wenzake walifanya promo interview ya show zao,Luther Akyoo
alikanusha Tunda Man kuwepo kwenye gari iliyopata ajali.
Taarifa
za Uhakika kutoka kwenye chanzo chetu cha habari (jina kapuni)zinadai
kuwa Man Katuzo ambae pia ni mwanamuziki,ndie aliekua promota wa show
ambazo Tunda Man alifanya mkoani Iringa hali iliyopelekea familia ya
marehemu kuchukizwa kwa kitendo cha Tunda Man kumuita marehemu
dereva,wakati akijua wazi wasifu wa marehemu,Man Katunzo.
Kilichowasikitisha zaidi watu ni kitendo cha Tunda kuamua kurudi Dar
es salam akitokea Iringa na kuuacha mwili wa marehemu na majeruhi
hospitali huku akidaiwa kuondoka na camera mbili mali za marehemu ambapo
mara baada ya tetesi za camera hizo kuchukuliwa na Tunda na wenzake
kuvuja,jeshi la polisi Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na jeshi la
Polisi Mkoa wa Morogoro walifanikisha kupekuliwa kwa gari alilokuwemo
Tunda Man na wenzake eneo la Mikumi,Morogoro ambapo mara baada ya
upekuzi walikutwa na camera hizo.Chanzo chetu cha habari kilienda mbali
na kudai kuwa achilia mbali urafiki ambao Tunda Man na Man Katuzo
walikua nao,Tunda Man hakufika kwenye msiba wa rafiki yake huyo kitendo
kinachoonesha ni kwa kiasi gani Tunda Man alivyokosa ubinadamu.
djwillkan.blogspot.com
No comments:
Post a Comment