Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Tanzania (CAG) Profesa Juma Musa Asaad
ameamua kuweka wazi mambo kadhaa kuhusiana na ripoti yake, kikubwa
alichozungumza mkaguzi mkuu kabla ya kuamini ripoti yoyote inayoandikwa
mitandaoni, unatakiwa uangalie vitu viwili muhimu ili kufahama kama
hiyo ni ripoti yake au la.
Ripoti inayotoka kwa CAG huwa ina vitu viwili muhimu vya kuzingatia ili uweze kujiridhisha na kufahamu, ripoti ya CAG ni lazima iwe na saini au kama itatolewa moja moja huwa ina muhuri wa kuthibitisha kuwa hiyo ni ripoti ya CAG. Hivyo ndio vitu viwili muhimu ambavyo vinaweza kukudhihirishia kuwa hii ni ripoti rasm ya CAG.
“Kwa
sababu unataka taarifa rasmi hivi ni vitu vya kuzingatia kuhusu ripoti
yangu, ripoti yangu tofauti yake ni kwamba inakuwa na saini na pia
ripoti zetu kama ikitoka moja moja inakuwa na muhuri wa kuthibitisha
kuwa hii ni ripoti rasmi”
UNGANA NAMI KATIKA MITANDAO MINGINE YA KIJAMII: Facebook== DJWillkan.com, Twitter== @Djkanvol Instagram== @djwillkan_zekanvol
KWA HABARI MOTOMOTO ZA KIBURUDANI, SIASA, MICHEZO, HABARI ZA KUSISIMUA NA ZINGINE NYINGI.
djwillkan.blogspot.com
No comments:
Post a Comment