Licha
ya kuwa washindani katika game ya mziki, Rapper Kanye West na familia
ya Carter, Jay Z & Beyonce wamekuwa marafiki wakubwa tu kwa muda.
Kanye West ameweka hilo pembeni na kufunguka kwamba hakupendezwa na
kitendo cha Beyonce kusema hato perform kwenye tuzo za MTV Video Music Awards 2016 endapo
video yake ya ‘Formation’ haitoshinda kama Video bora ya mwaka. Kanye
aliyasema hayo alipokuwa kwenye show yake huko Sacramentino Carlifonia.
Beyonce alikuwa akishindanishwa na Kanye West pamoja na Drake
kwenye kipengele hicho ambacho hata hivyo, alishinda. Kanye alisema
alijisikia vibaya kusikia vile tena kama utakumbuka Kanye alishawahi
kuingilia speech ya Tailor Swift mwaka 2009 alipopokea tuzo ambayo
alisema alistahili kuchukua Beyonce kitu ambacho kilimfanya asiwe na
mahusiano mazuri na Taylor Swift.
Kanye aliendelea kwa kusema “sijaongea
hivi ili muende kumdiss Beyonce, Beyonce ni mtu mahiri na hata Taylor
Swift pia, mimi naongea tu mawazo yangu japokuwa wakati mwingine siasa
zinatupelekea kujisahau”. Kanye alimalizia kwa kumsihi Jay Z amcheki hewani waongee kama wanaume.
Baada ya
kusema hayo Kanye alitupa Mic chini na kuondoka kwenye steji, kitu
ambacho kililalamikiwa na mashabiki huku wakisema hawakwenda kutazama
show ya nyimbo mbili tu.
No comments:
Post a Comment