Wednesday, December 7, 2016

Muziki wa Trap sasa umekuwa tishio kwa Lugha ya Kisukuma. NKUNDA STAR,..Hii kutokea Shinyanga.

Mwanamuziki wa Bongo Fleva na muziki wa Trap, Erick John maarufu kwa jina la NKUNDA STAR, kutokea Shinyanga. Amejinyakulia umaarufu kwa muda mchache tu baada ya kutengeneza nyimbo iliyoimbwa kwa beat ya trap na kuweka maneno kwa lugha ya Kisukuma.
DIMAGA ndilo jina la wimbo huo ambao hadi kufikia sasa amejinyakulia mashabiki wengi sana ndani ya Mkoa wa Shinyanga na mikoa mingine mingi ndani Tanzania na nje pia. Kwa sasa akiwa katika harakati za kushoot video na kuutambulisha rasmi kwa mashabiki.
Dj Willkan Blog ilimvutia waya Mwanamuziki huyo na kumuhoji kwanini nyimbo hiyo imekuwa masikioni mwa watu na wakati bado haijatambulishwa rasmi?

Alijibu kama ifuatavyo: Kupitia kipindi kinachorushwa na kituo cha television cha Clouds Tv (Siz kitaa), nadhani kimekuwa miongoni mwa kipindi ambacho kimenipush sana kwa namna moja ama nyingine.
Casto Dickson & Nkunda Star (siz kitaa)
Swali: Tutegemee lini kuisikia Dimaga katika Vituo mbalimbali?....................Majibu yake hayakuonesha ni lini ataiachia ngoma kali DIMAGA .

Endelea kuitembelea DJ WILLKAN BLOG
kwa kulike Page yetu ya Facebook,..DJWillkan.com, pia Instagram:@ djwillkan_zekanvol
tufollow pia Twitter: @Djkanvol

No comments:

Post a Comment