![]() |
Barnaba |
Barnaba amefunguka kuhusiana na mahusiano yake na mama Steve kwa sasa.
Wiki chache zilizopita muimbaji huyo alidaiwa kuachana na mzazi mwenzake huyo ambaye wamefanikiwa kupata mtoto mmoja.
Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, hitmaker huyo wa Lover
Boy amesema, “Kwa sasa siko kwenye maelewano mazuri na mama watoto
wangu. Sio kwamba tumeachana au tumetengana sitaki kusema hivyo.”
“Siwezi kusema simpendi mwanamke niliyepata nae mtoto [mama
Steve],yule ameshakua kama ndugu yangu.Namrespect sana mama Steve ila
kila mtu anaendelea na maisha yake na hatutaki kutengeneza picha mbaya
kwa mwanetu,” ameongeza.
Wakati huo huo Barnaba amesisitiza kuwa wimbo wake mpya wa ‘Lonely’
ambao ameuachia leo haujamgusa mtu yoyote na wala hausiani na maisha
yake.
CHANZO CHA HABARI NA:teamtz.com
Endelea kuitembelea DJ WILLKAN BLOG
kwa kulike Page yetu ya Facebook,..DJWillkan.com, pia Instagram: @djwillkan_zekanvol
tufollow pia Twitter: @Djkanvol
No comments:
Post a Comment