Saturday, December 13, 2014

KUSHINDANIA TUZO ZA HMA 2015,...DIAMOND NA OMMY DIMPOZ


Ommy Dimpoz na Diamond wakipeana mkono wa kheri

Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Diamond Platinum na Ommy Dimpoz wametajwa kuwania tuzo za muziki za nchini Uganda ziitwazo HiPipo Music Awards (HMA) 2015 zinazotarajiwa kutolewa rasmi February 07, 2015.

Diamond na Dimpoz watachuana katika kipengele kimoja cha ‘East Africa Super Hit’ kupitia nymbo zao Ndagushima na Number One original.

Katika kipengele hicho wakali hao watachuana na Sauti Sol, Jaguar, Eddy Kenzo, Baramushaka, Urban Boys na Bebe Cool.

Aidha, hatua hiyo inaonesha jinsi muziki wa Bongo flava unavyoendelea kufanya vizuri katika soko la muziki la kimataifa na jinsi unavyokubalika kwa kasi kubwa.
 
 
djwillkan.blogspot.com

No comments:

Post a Comment