Staa wa Bongo Fleva na Bongo Movie, Shilole ataka kumpiga tena mpenzi wake ambaye pia ni Msanii wa Bongo Fleva Nuh Mziwanda, kwa chupa hivi karibuni wakiwa kwenye Sherehe ya kuzaliwa ya Meneja wake na Kajala, aitwaye Lamata, iliyofanyika Samaki Samaki, Posta Jijini Dar.
Inavyosemekana Shilole alikuwa amelewa sana na walikuwa wamekaa sehemu tofauti yeye na Mziwanda, Nuh Mziwanda alikuwa amekaa na Wasanii wengine. Mara ghafla chupa ilirushwa eneo lile mkilenga Mziwanda, bahati nzuri aliikwepa na kumpiga jamaa mwingine lakini haikumjeruhi.
Baadhi ya Wasanii walitaka kujua chanzo ni nini lakini mpaka kutaka kumpiga Mpenzi wake Nuh Mziwanda, Shilole hakusema kitu na badae akaenda pembeni pekeake na kuanza kulia. Wakati akilia Quick Racker alimsogelea na kuanza kumwambia kumbe ukilia unakuwa mbaya, Shilole alinyanyua tena chupa nyingine na kumrushia Quick Racker, Quick Racker bahati nzuri na yeye aliikwepa.
No comments:
Post a Comment