Deborah Oluwaseyi Joshua ni msanii kutoka Nigeria anayefahamika zaidi kwa jina la Seyi Shay. Seyi Shay
ni mtunzi nyimbo, recording artist, performer na producer wa muziki
aliyekulia Uingereza. Ameshwahi kuwandikia wasanii kadhaa nyimbo ikiwemo
Wale, Chipmonk na Ne-yo.
Safari yake kimuziki ilianza kwenye kundi la muziki From Above lililokuwa lina simamiwa na Matthew Knowles baba wa RnB Superstaa Beyonce Knowles, akiwa chini ya kundi hilo walifanikiwa kusign mkataba na kampuni kubwa ya kurekodi, Sony/Columbia manger wao akiwa Matthew Knowles.
Kwenye interview moja aliofanya Seyi Shay alikaa na kuzungumzia changamoto pamoja na fursa alizozipata kupitia Industry ya muziki, Seyi Shay alikuwa na haya ya kusema:
>>>“Changamoto
zipo nyingi, nimeshawahi kuimba mpaka nikahisi koo inanitoka lakini
hakuna hata mtu mmoja alienipigia kelele wala makofi kwenye hiyo show,
nimeshawahi kuanguka stejini na nikachekwa sana ila show ilibidi
iendelee, sometimes nguo zangu stejini ziliachia na kunifanya
nisimamishe performance hiyo kujiweka sawa.<<< Seyi Shay”.
>>>“Nilivyorudi
Nigeria kutoka Uingereza nilipata changamoto nyingi haswa kuingia
kufanya mziki Nigeria, ila kilichonisaidia nilikuwa tayari nimeshajengwa
kuwa msanii so nilipopata team yangu nilioridhika nayo changamoto
nyingi zilipungua”. Seyi Shay
>>>
“Kwenye upande wa fursa, nimepata fursa nyingi kwenye industry ya
muziki, kabla ya kuanza rasmi kuimba solo nilishawahi kuwa mmoja ya
madansa wa Beyonce na chini yake tulitembea dunia na kufanya shows
nyingi sana, alinifundisha mengi yaliyonijenga kama msanii, pia nimepata
fursa ya kutembea dunia na kufanya shows nyingi”.
>>>“Nimeshawahi
pia kumuandikia Wale nyimbo na kushare nae stage moja, nimeshare stage
na Rick Ross, Wizkid, Fuse ODG na wengine. Pia nlishawahi kuwa kwenye
kundi la muziki lililoitwa From Above wasichna 5 waliochaguliwa na baba
yake Beyonce, alitupa training na kutumange kama kundi nae pia
alinifundisha mengi kuhusu muziki na mpaka leo bado tunawasiliana”.
No comments:
Post a Comment